Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ujerumani wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi baada ya kuilaza Ireland Kaskazini mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa mjini Belfast.
Ujerumani walitangulia kupata bao kupitia Sebastian Rudy mnamo dakika ya pili kabla ya Sandro Wagner kuongeza bao la pili na baadaye Joshua Kimmich akafunga la tatu mchezo ukikaribia kumalizika.
Bao pekee la Ireland lilifungwa na Josh Magennis aliyefunga kwa kichwa dakika za lala salama.
-
Kane aipeleka Uingereza kombe la dunia
-
Pogba marufuku kucheza mpira wa kikapu
-
Argentina, Uruguay kuandaa kombe la dunia 2030
Tazama magoli yalivyofungwa katika video hii hapa chini;