Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ujerumani wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi baada ya kuilaza Ireland Kaskazini mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa mjini Belfast.

Ujerumani walitangulia kupata bao kupitia Sebastian Rudy  mnamo dakika ya pili kabla ya Sandro Wagner kuongeza bao la pili na baadaye Joshua Kimmich akafunga la tatu mchezo ukikaribia kumalizika.

Bao pekee la Ireland lilifungwa na Josh Magennis aliyefunga kwa kichwa dakika za lala salama.

Tazama magoli yalivyofungwa katika video hii hapa chini;

Breaking News: Mshindi wa Tuzo ya Nobel 2017 atangazwa
Video: Polisi Dar waendelea na uchunguzi wa waliofariki kwa pombe