Polisi jijini Mumbai nchini India wamewalaumu panya kwa kutoweka kwa kilo 34 za dawa za kulevya zijulikanazo kwa jina la Ketamine
Wamesema kuwa wanawalaumu panya hao baada ya kukuta magunia hayo yametobolewa kwa chini hivyo kusababisha kupungua kwa dawa hizo ambazo zilikuwa zimehifadhiwa.
Aidha, Dawa hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala la serikali zilikuwa miongoni mwa kilo 200 za mihadarati zilizokuwa zimekamatwa kutoka kwa wafanyabiashara wa mihadarati hiyo mwaka 2011.
Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa jeshi la polisi nchini India kuwalaumu panya hao kwa kutoweka ulinzi wa kutosha katika mihadarati iliyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa na kuhifadhiwa katika ghala la serikali.