Siku chache baada ya watu katika jimbo la Catalonia kuandamana kushinikiza kujitenga na Hispania, wale wanaopinga juhudi za jimbo hilo kujitenga leo wamepanga maandamano makubwa huko mjini Madrid wakisema Hispania ni taifa moja na hawataki ligawanyike.

Hatua hiyo inakuja baada ya watu wa jimbo la Catalonia kupiga kura ya kutaka kujitenga na kutangaza uhuru wao ambapo hata hivyo utawala wa serikali kuu ulitumia nguvu na mbinu tofauti kujaribu kuzuia kura hiyo.

Mzozo huo umesababisha wasiwasi mkubwa sio tu wa kisiasa bali pia wa kibiashara ambapo mapema leo benki ya pili kuu Caixabank, imetangaza kuondoa makao yake makuu kutokana na wasiwaasi unaoendelea kuligubika eneo hilo.

Hali ya kiuchumi ilnaelekea kuwa ya wasiwasi kwani shirika la fedha dunia ,IMF limesema mzozo huo unaharibu mazingira ya uwekezaji wa Catalonia.

Ni dhahiri pande zote mbili na hata jamii ya kimataifa zingependa kuona mzozo huo umesuluhishwa kwa majadiliano lakini bado hamna dalili zozote kwamba yatafanyika hivi karibuni.

Bayern Munich yamrejesha Jupp Heynckes
Video: Kashililah ang'olewa Ukatibu wa bunge