Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na Waziri wa Uwekezaji wa Oman, Salim Al Ismail wamejadili suala la uwekezaji wa viwanda katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi.

Mawaziri hao wamekutana na kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya viwanda vya nyama ili kuweza kufufua biashara ya nyama kati ya nchi ya Tanzania na Oman. na kuendeleza viwanda vidogo vidogo vilivyopo.

“Tunataka viwanda vyote vya nyama vya ndani vikidhi mahitaji na kuweza kuuza nyama nje ya nchi, hasa katika falme za kiarabu ambapo wamekuwa wanunuzi wakubwa wa nyama kutoka Tanzania,”amesema Mpina.

Kwa upande wake Waziri wa uwekezaji wa Oman, Salim Al Ismail amesema kuwa, Oman ipo tayari kuwekeza katika sekta ya viwanda vya nyama na kuisaidia Tanzania kutafuta soko katika nchi za Amerika kupitia Oman kwani nchi hiyo ina kibali kilichothibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa cha nchi hizo.

“Tunaweza kuchukua nyama kutoka Tanzania na kuingiza Marekani bila kulipa Ushuru, tunapaswa kuwa na vyeti halali ili kuweza kupata soko katika nchi nyingine,”, Amesema Waziri Ismail

Hata hivyo, Waziri huyo ameongeza kuwa makampuni binafsi kutoka Oman yako tayari kufanya biashara katika eneo hili hivyo ni wakati wa Tanzania sasa kuonyesha utayari.

 

Birdman wa Cash Money kufanya ziara Tanzania
Ebitoke afunguka chanzo kikuu cha kuachana na Ben Pol