Mchekeshaji wa kike, Ebitoke amesema kuwa kukosa muda wa kutosha wa kuwa karibu na Ben Pol ni sehemu ya chanzo cha wawili hao kuachana.

Msanii huyo ameeleza kuwa aliamua kufungua ukurasa mpya baada ya kubaini kuwa hakukuwa na mapenzi ya kweli kati yao na kwamba muda mwingi amekuwa akikosa furaha na amani.

“Unajua mapenzi ni hisia na yanahitaji sana furaha sasa mimi niligundua kama ninamlazimisha Ben Pol, hivyo nikaamua kumuacha aendelee na maisha yake ya kawaida,” Ebitoke aliiambia Papaso ya TBC FM.

“Yeye ndiye aliyeanza kuniacha kwani muda mwingi alikuwa anasema yupo ‘bize’ na mimi nikasema basi ngoja nifanye vitu vyangu maana mwenyewe pia nina ndoto zangu nyingi tu, japo nilikuwa naumia lakini sasa hivi nina furaha na maisha haya mapya,” alifunguka.

Ebitoke na Ben Pol waliweka wazi kuwa na uhusiano wa mapenzi na walionekana mara kadhaa kwenye matamasha makubwa wakifuatana kama ‘ndege tetere’.

Lakini hivi sasa, Ebitoke amekuwa akifunguka kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wao wakati Ben Pol akiwa kimya juu ya suala hilo.

Oman kuwekeza katika viwanda vya nyama nchini
Mahaba Niue: Huddah amfungukia Jux