Manchester City imeahirisha mpango wake wa kumsajili Alexis mwezi katika dirisha la usajili la mwezi Januari na kuamua kusubiri mpaka mwisho wa msimu huu huku klabu ya Everton nayo ikionyesha nia ya kumuhitaji mshambuliaji huyo raia wa Chile.
Pep Guardiola alitangaza ofa ya Pauni milioni 60 kutaka kumsajili Sanchez muda mfupi kabla ya dirisha la usajili kufungwa lakini Arsenal walikataa ofa hiyo kwani ilikuwa ngumu kupata mbadala wake ikiwa ni muda mfupi kabla ya tarehe ya mwisho ya kufunga usajili mwezi Agosti.
Wakati City wakionyesha kuwa na subira juu ya usajili wa Sanchez mmiliki wa klabu ya Everton, Farhad Moshiri ameonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
-
Yanga, Simba zatoka suluhu huku Kichuya akiweka rekodi ya aina yake
-
Anthony Joshua amtwanga Carlos Takam
-
Moto wa Man City hauzimiki, Liverpool, Arsenal nao kifua mbele
Moshiri anataka kumuona Sanchez akitua Goodison Park lakini huenda ikawa ngumu sana kwani mchezaji huyo anataka kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya ‘UEFA Champions’ jambo ambalo kwa klabu kama Everton litakuwa gumu.
Klabu za Bayern Munich na Paris Saint-Germain pia zilitaka kumsajili Sanchez kalba ya mchezaji huyo kutaka kiasi cha mshahara mkubwa wa pauni 500,000 kwa wiki ikiwa ni kwa makusudi ya kutaka kuwakatisha tamaa nia yake ikiwa ni kwenda Man City.