Chama tawala Zimbabwe ZANU PF kimemtaka Rais Robert Mugabe ajiuzulu. Gazeti la Herald nchini humo limeandika kuwa matawi ya chama hicho katika majimbo yote10 yalikutana na kumtaka Rais huyo kujiuzulu.

Viongozi wa chama hicho wamesema kuwa wataendelea kumshinikiza kiongozi huyo ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 kuondolewa kutoka kwenye uongozi wa chama hicho ifikapo hapo kesho Jumapili, na baada ya hapo, bunge litapiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Aidha, Mugabe alionekana kwa mara ya kwanza hadharani, katika mahafali ya chuo kikuu cha Harare siku ya Ijumaa tangu jeshi lilipomuweka kizuizini nyumbani kwake.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya jeshi la Zimbabwe imesema kuwa viongozi wake bado wanashauriana na Rais Robert Mugabe kuhusu njia bora ya kuweza kuondokana na mgogoro huo wa madaraka ikiwemo kumtaka rais huyo kung’atuka madarakani.

 

Halmashauri zapigwa marufuku kuingia makubaliano na NGO's
Kikosi cha Kilimanjaro Stars chatajwa