Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Ammy Ninje ametaja majina 20 ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu hiyo itakayoshiriki michuano ya CECAFA Challenge mwaka huu.

Kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 27 mwaka huu kujiandaa na michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu nchini Kenya.

Aidha, kikosi hicho kinaundwa na makipa, Aishi Manula na Peter Manyika,wakati walinzi ni Boniphace Maganga, Gadiel Michael, Kevin Yondan na Erasto Nyoni. Wengine ni Mohamed Husein na Kennedy Wilson.

Viungo ni Himid Mao, Hamis Abdallah, Mzamiru Yassin na Rafael Daudi. Wengine ni Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib na Abdul Hilal, huku washambuliaji ni Elias Maguli, Mbaraka Yusuph, Yohana Mkomola na Daniel Lyanga.

ZANU PF yamshinikiza Rais Mugabe kujiuzulu
Watuhumiwa dawa za kulevya kuhukumiwa jela maisha