Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amesema kuwa yeye bado ni kiongozi halali wa nchi hiyo na kukataa upatanishi unaofanywa na Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki ili kuwezesha mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani baada ya jeshi kuchukua udhibiti tangu siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini humo, Kasisi Fidelis Mukonori, amejitolea kuwa mpatanishi kati ya Majenerali wa Jeshi na Rais Mugabe, ingawa hakuna taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo yenye lengo la kuepusha umwagaji damu baada ya Mugabe kuondoka madarakani.

Aidha, taarifa zaidi zimesema kuwa Makamu wa Rais aliyetimuliwa, Emmerson Mnangagwa, amekuwa akiandaa mpango wa uongozi baada ya Mugabe kuondoka madarakani akishirikiana na jeshi pamoja na upinzani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Hata hivyo, kiongozi wa chama cha upinzani nchini humo cha MDC, Morgan, Tsvangirai, ambaye amekuwa akipatiwa matibabu ya Saratani nchini Afrika Kusini na Uingereza amerejea Zimbabwe na kumtaka Rais Mugabe kung’atuka kwa amedai kuwa ameishiwa uwezo wa kuiongoza nchi hiyo

 

 

Prof. Kitila Mkumbo ajiunga rasmi CCM
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 17, 2017