Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewateua wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Disemba 1 2017.
Mwijage amefanya uteuzi huo baada ya Rais Magufuli kufanya uteuzi kwa Prof. Egid Beatus Mubofu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania.
Aidha bodi hiyo inategemea kuzinduliwa tarehe 11 mwezi mwezi wa kumi na mbili katika wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji mjini Dodoma.