Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini kuteketeza mali zake zote endapo atahama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuhamia CCM.

Amesema hayo wakati akiwatumia salamu wale ambao wamekuwa wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kuwa heshima na dhamana aliyopatiwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni kuuza hadi utu wa wapiga kura.

Ameweka wazi kuwa amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka upande wa chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama na bila hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020.

“Walianza kunipigia kwa kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani” I am not that ‘cheap’ wakatafute wengine,”amesema Msigwa

Hata hivyo, Msigwa ameongeza kuwa hakuingia bungeni kwasababu anahitaji pesa kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa makampuni na kuongeza kuwa alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa mwanasiasa na mbunge.

 

ANC wakutana kumchagua mrithi wa Zuma
Zitto aipigia chapuo Zanzibar Heroes