Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa anamatumaini makubwa ya kufungua ubalozi wa Uturuki katika taifa la Palestina ndani ya Jerusalem Mashariki.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wafuasi wa chama chake katika mji wa Karaman, ambapo amesema kuwa sababu kubwa ya kufungua ubalozi huo ni kuweza kuipa nguvu Palestina ambayo kwasasa inakaliwa kimabavu na Israel.

“Inshallah, siku zinazidi kukaribia, tutafungua ubalozi huko Palestina ili kuweza kuwaunga mkono Wapalestina ambao wanataka kupokonywa mji huo,”amesema Erdogan

Aidha, hatua hiyo imekuja mara baada ya Erdogan kufanya mkutano na viongozi wa mataifa yenye waislamu wengi, kupinga uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Hata hivyo, Uturuki kwa hivi sasa ina ubalozi mdogo Jerusalam, na ina uhusiano kamili wa kibalozi na Israel ikiwa ni pamoja na kuwa na ubalozi kamili mjini Tel Aviv kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani.

 

Video: Lissu amsubiri ndugai kwa hamu, Mangula arudishwa
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 18, 2017