Jeshi la Nigeria limesema kuwa limefanikiwa kumuokoa msichana mmoja aliyekuwa anashikiliwa na kundi la kigaidi la Boko Haram tangu mwaka 2014.
Kupitia taarifa yake kwa umma, Jeshi hilo limeeleza kuwa lilimuokoa msichana huyo katika eneo la Pulka jimbo la Borno mpakani mwa Cameroon.
“Kwa sasa, msichana huyo ambaye alikuwa anaambatana na msichana mwingine mdogo mwenye umri wa miaka 14, kwa pamoja wako salama katika hifadhi ya jeshi na wanapatiwa matibabu,” taarifa hiyo ya jeshi inakaririwa na BBC.
Mwaka 2014, kundi la Kigaidi la Boko Haram liliwateka na kuwashikilia wasichana 200 waliokuwa wanafunzi katika eneo la Chibok, Kaskazini mwa nchi hiyo.
- Ashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli
- Video: Makamba, Dkt. Tulia, Polepole wamlilia mke wa Naibu Waziri Kangi Lugola
Baadhi ya wasichana walifanikiwa kutoroka, wengine waliachiwa huru na kundi hilo kutokana na makubaliano na Serikali ya Nigeria lakini wengine wanaendelea kushikiliwa na magaidi hao.
Nigeria na Cameroon wanashirikiana katika mpaka wa nchi hiyo kupambana na kundi hilo.