Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka jamii kuondokana na dhana potofu ya kuhusisha ugonjwa wa ukoma na imani za kishirikina.
meyasema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mtu anapopatwa na dalili za ugonjwa huo anapaswa kutafuta tiba mapema na si vinginevyo.
Amesema kuwa wastani wa wagonjwa 2040 huugua ukoma kila mwaka wakiwemo watoto na vijana ambao hufika hospitali wakiwa tayari wameshapata ulemavu.
“Ukoma ni ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya hewa, hauna uhusiano wowote na ushirikina, na unapohisi mwili wako uko tofauti wahi hospitalini ukapate tiba,”amesema Dkt. Ndugulile