Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu (TCC) kusimamia na kuhakikisha Walimu wote wanapanda madaraja kwa wakati na kwa mujibu wa Elimu zao ili kupunguza Malalamiko yao Nchini.

Ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Tume za Utumishi wa Walimu za Wilaya kwa Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilichopo Mkoani Dodoma mapema leo.

Asema kuwa kumekuwa na malalamiko, manung’uniko na masononeko ya muda mrefu toka kwa Walimu kuhusu suala hilo la upandaji wa madaraja kuwa halifuati taratibu.

‘Tume hii ifanye kazi ya kurudisha hadhi ya Walimu, iwajengee heshima na thamani yao katika Jamii, shughulikieni malalamiko yao ya Msingi madaraja yao yapande kwa kuzingatia muda waliokaa kazini, elimu yao na Utendaji wao wa kazi; hilo lisitegemee “favour” ya Katibu wa Watumishi wa Tume waliopo katika eneo husika,”amesema Jafo

Hata hivyo, Jafo amewasisitiza wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu kuwa Mkutano huo utumike kupeana maarifa ya kazi, jinsi gani mnaweza kufanya kazi kwa usahihi zaidi kwa kuzingatia sheria iliyounda TUME YA UTUMISHI WA WALIMU ya mwaka 2015 na Kanuni zake za mwaka 2016.

JPM amchangia mamilioni Wastara
Nikki wa Pili akanusha alichohoji Nassari