Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janet Magufuli wamemchangia muigizaji wa filamu Tanzania, Wastara Juma shilingi milioni 15, kumsaidia katika matibabu yake.

Mchango huo umekabidhiwa kwa Wastara na Katibu wa Rais, Ngusa Samike , sambamba na kiasi kingine cha milioni moja na laki tisa ambayo ni michango kutoka kwa wasaidizi wa Rais.

Aidha, Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na mguu kwa muda mrefu na alikuwa akiomba msaada kwa Watanzania mitandaoni ili aweze kwenda nchini India kupatiwa matibabu.

Hata hivyo, Rais Magufuli anakuwa mtu wa kwanza kutoa fedha nyingi kwa msanii huyo, tangu aanze kutoa rai ya kuomba michango, ambapo wiki iliyopita Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo Dkt. Harison Mwakyembe alimkabidhi shilingi milioni moja

Video: Wastara akikabidhiwa milioni 15
Jafo aitaka tume kurudisha hadhi ya Walimu