Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga amemuomba radhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya watu wa Iringa kwa kukosa kura 25 za udhamini katika kipindi cha kampeni za uchaguzi 2015.

Ameyasema hayo leo Mei 1, 2018 kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa inayofanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kulenga uboresha mafao ya wafanyakazi.

“Nakumbuka Mhe. Rais ulipata shida kidogo kupata wadhamini hapa Iringa Mjini ikabidi utoke nje ya mji ndiyo ukapata, ila wadhamini 25 kwa hapa mjini kura hazikupatikani tunakuomba radhi sana,”amesema Mahiga

Hata hivyo, Mahiga amemshukuru rais Dkt. Magufuli kwa kuchukua maamuzi ya kuitengeneza barabara ya kutoka Iringa mjini kwenda katika hifadhi ya Ruaha kwani itaongeza tija kwa jamii.

 

 

Mzee Majuto kusafirishwa India leo
Marekani yaituhumu Iran kuvuruga amani ya Mashariki ya Kati