Msanii wa filamu bongo, Mchekeshaji Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto leo hii anatarajia kusafirishwa kuelekea nchini India kwa ajili ya matababu zaidi kufuatia matatizo aliyopata siku kadhaa zilizopita.

Awali Mzee Majuto alilazwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es saalam kwa matibabu zaidi ya kidonda alichofanyiwa upasuaji na kumletea shida ambapo mnamo Januari 2018, Majuto alifanyiwa upasuaji wa Tezi dume.

Steve Nyerere ambaye amehusika kusaidia kuratibu zoezi la kumuwezesha Mzee Majuto kwenda nchini India kwa matibabu zaidi amefunguka na kusema kuwa leo Mzee huyo atakwenda kwa matibabu zaidi nchini India na kuwataja watu ambao wamehusika katika kufanikisha jambo hilo na kusema ni pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe.

Niseme ahsante sana Mhe. Rais John Pombe Magufuli, Mhe. Mwakyembe, Ummy Mwalimu na wadau pamoja na wasanii mbalimbali kwa kujitoa kwenu, Mzee wetu King Majuto Mungu akipenda leo atakuwa njiani kwenda India kwa matibabu zaidi” .

Aidha kupitia Mzee Majuto Waziri wa tasnia hiyo, Dk Harrison Mwakyembe amechukua fursa hiyo kutoa msaada wa kisheria kwa wasanii wote ambao wamesainishwa mikataba mibovu na kufanya kazi na makampuni makubwa.

Na katika kulitelekeza hilo Mwakyembe amesema ataanza kushughulikia mikataba ya Majuto na Marehemu Kanumba ili waone wapi walionewa na waweze kupata haki yao.

 

 

Steve Nyerere ataka wasanii kumiliki bima, ''tutakuwa watu wa kuomba msaada''
Waziri ampigia magoti JPM, asema yaliyopita si ndwele