Bunge la Rwanda limeidhinisha muswada unaowataka wachungaji wa makanisa kuwa na shahada ya theolojia pia imeyataka madhehebu yote nchini humo kuweka wazi vyanzo vya fedha za matumizi ikiwemo sadaka na michango wanayoipata kutoka kwa wadhamini.
Hatua hiyo ni kufuatia serikali kufunga makanisa 1000 mwanzoni mwa mwaka huu, kwa kushindwa kutimiza vigezo na kanuni za ujenzi.
Yves Bucyana, mwandishi wa BBC amesema kipengele cha 20 kuhusu ulazima kwa anayetaka kufundisha neno la Mungu nchini Rwanda kuwa na shahada ya theolojia kilizua mjadala mkali huku baadhi ya wabunge wakitaka fedha hizo kukatwa ushuru.
“Hapa Rwanda mtu yeyote aliye na kipato cha elfu 30 hulipa ushuru, hawa watu wa makanisa wakipokea michango ya milioni tano au 10 hawalipi ushuru. Nahoji hawa wenye kipato kikubwa kwa nini pia wao wasilipe ushuru?, ni jambo lisiloeleweka.” Alisisitiza mmoja wa wabunge.
-
Mahakama yalitoa MwanaHalisi kifungoni, lakutana na kiunzi kingine
-
TRA yawataka wafanyabiashara kuacha kulalamika
Hata hivyo watu mbalimbali walitoa maoni yao wakidai sheria hiyo inaingilia haki na uhuru wa madhehebu kwani uwezo wa kufundisha neno la Mungu ni wito na kipaji zaidi kutoka kwa Mungu na si kisomo cha darasani.
”kuna watu ambao wanaitikia mwito wa Mwenyezi mungu bila ya wao kupitia shule yoyote.Kama Petro hakusoma shule yoyote.Yesu alimkuta akiwa mvuvi wa samaki.Paulo alikuwa msomi,lakini Yesu Christo hakuwahi kusoma. Je waweza kuniambia chuo ambacho Yesu alisomea?”. Alisema Mchungaji mmoja
Lakini wengine wanahisi kwamba ni vyema wachungaji wawe na elimu ya theolojia na kwamba kuwepo kwa vyuo vikuu vinavyofundisha taaluma hiyo kunadhihirisha umuhimu wake.
Aisha, sheria mpya makanisa inasema kwamba kanisa litakuwa ni nyumba kubwa yenye kufuata kanuni zote za ujenzi wa kisasa, ikiwemo vidhibiti sauti kwa ajili ya usalama wa majirani na kwamba sala zinazoendeshwa kwenye mapango,milimani au jangwani haziruhusiwi.