Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara umekamilika kwa asilimia 98 na itafunguliwa Oktoba mwaka huu na Rais Dkt. John Magufuli.
Mradi wa barabara ya juu (Mfugale flyover) chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani, unalengo la kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere.
Ameyasema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo wa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar Es Salaam.
“Mradi huu utapunguza muda wa usafiri katika barabara ya Nyerere hususani kwa wananchi wanaotoka katikati ya jiji kwenda uwanja wa ndege na wanaotoka Buguruni, Temeke.”amesema Majaliwa
Katika hatua nyingine, Majaliwa amewaagiza viongozi Mkoa wa Dar Es Salaam watafute eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo ili waweze kuondoka kandokando ya barabara hizo za juu zinazojengwa.
-
Benki ya Standard Chartered kuipatia mkopo Tanzania
-
Video: Bahati nzuri kwangu sijafa, bahati mbaya sana kwao sijafa- Tundu Lissu
-
Ndalichako: Hatutoi mabilioni ya fedha watoto wakapoteze maisha shuleni
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ujenzi wa mradi wa barabara ya juu katika eneo la Tanzara (Mfugale flyover) unagharimu sh. bilioni 100.52 na unajengwa na kampuni ya Sumitomo Mitsui ya nchini Japan.