Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa utawala wa sasa haujali haki za binadamu kwa sababu kuna hofu kubwa imetanda kwa viongozi wa upinzani.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na BBC nchini Ubelgiji anakopatiwa matibabu tangu kupigwa risasi na watu wasiojulikana mwaka jana.

Amesema kuwa, upinzani unakabiliwa na wakati mgumu sana chini ya utawala wa awamu ya tano. tofauti na tawala zilizopita.

“Wapinzani hatujakaa kimya, viongozi wa upinzani wanapigania maisha yao, tuna familia. huwezi kama unaambiwa uwe mahakamani kila siku ili ujitetee, muda wa kwenda kufanya kazi nyingine unakuwa haupo. lakini kusema kweli hatujanyamaza na tunakabiliana na ukatili mkubwa sana ambao haujawahi tokea,”amesema Lissu

Gianni Infantino, Donald Trump wakutana kwa mara ya kwanza
Esma auponda wimbo wa Hamisa adai aache kuomboleza