Jeshi la Polisi Nchini Ethiopia limesema kuwa limegundua kaburi la watu wengi lililokuwa na miili ya watu takribani mia mbili karibu na mpaka kati ya majimbo ya Oromia na Somalia.

Mamia kwa maelfu ya watu wameyahama makazi yao katika kipindi cha mwaka uliopita kutokana na ghasia katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la FANA nchini humo, polisi imegundua kaburi hilo la watu wengi wakati ikifanya uchunguzi juu ya madai ya ukatili uliofanywa na Rais wa zamani wa Ethiopia katika mkoa wa Somalia.

Aidha, rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdi Mohammed alilazimika kujiuzulu nafasi ya urais wa nchi hiyo, August mwaka huu na kushikiliwa kifungoni akisubiri hukumu dhidi ya madai hayo, ya kuchochea mapigano ya kikabila karibu na mpaka wa Somalia na mikoa ya Oromia.

Kikosi cha polisi kinachojulikana kama Liyu kinadaiwa kufanya mauaji hayo huku wakimpa taarifa Rais wa zamani wa nchi hiyo.

Hata hivyo, kwasasa Polisi wanajaribu kuitambua miili hiyo mia mbili iliyogunduliwa katika kaburi la pamoja.

 

JPM amtumbua balozi wa Tanzania nchini Canada
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 9, 2018