Bila shaka utakubaliana nami kwamba hakuna afya bila kuwa na afya ya akili, na ili kukusaidia kukabiliana na mafadhaiko na changamoto za kila siku katika maisha yetu yaliyojaa changamoto mbalimbali, hapa nakupa vidokezo 10 vya kuboresha yako.
Lakini kwanza, ni lazima kufahamu kwamba Afya ya akili inahusu ustawi wako wa kisaikolojia kwa ujumla ikijumuisha jinsi unavyojisikia, ubora wa mahusiano yako na uwezo wako wa kudhibiti hisia zako na kukabiliana na matatizo.
Mtu yeyote, anaweza kupata matatizo ya afya ya akili au kihisia na katika maisha huku wengi wetu watapata tatizo hilo kwa mfano hapa kwetu Tanzania watu watano kati ya watu 10 ni lazima watakuwa wanaishi na tatizo ya Afya ya akili.
Hivyo basi, vidokezo hivi vinaweza kukusaidia kuinua hali yako, kuwa mtulivu zaidi na kufurahia maisha kila wakati.
1. Boresha mahusiano yako ya kijamii, hasa ya ana kwa ana.
Simu na mitandao ya kijamii ina nafasi yake, lakini mambo machache yanaweza kukushinda nguvu ya kupunguza mfadhaiko, kukuongezea hisia za maumivu wakati uwezo wa kupata ahueni upo kwa kutumia njia bora ya kukutana ana kwa ana na watu wengine, hasa wale unaowapenda na watu wanaokutia nguvu.
2. Endelea kufanya kazi.
Kuwa ‘active’ kazini ni vizuri kwa ubongo wako kama ilivyo kwa mwili. Mazoezi ya kawaida ama shughuli mbalimbali zinaweza kuwa na athari kubwa kwa afya yako ya akili na kihisia, lakini ili kupunguza mkazo, kuboresha kumbukumbu, inakubidi kufanya kazi kwa weledi huku ukiifurahia nahii itakusaidia kulala vizuri na kupata afya njema pia.
3. Zungumza na mtu.
Ongea na watu kwa uso wa kirafiki. Ikiwa una wasiwasi, mfadhaiko au vinginevyo jaribu kufanya jambo hilo hasa kwa mtu ambaye unajua fika anajali, hii ni mojawapo ya njia bora zaidi za kutuliza mfumo wako wa neva na kupunguza mfadhaiko.
4. Heshimu hisia zako.
Kila mtu hupata ingizo la hisia zake mwilini kwa njia tofauti, hivyo ili kufurahisha hisia zako sikiliza nafsi inataka nini juu ya kile ambacho kitakupa unafuu, nakushauri pendelea kupata utulivu kwa kukaa kivulini huku ukisikiliza sauti nzuri za ndege na kufurahia upepo unaovuma na pia penda kufanya matembezi ya peke yako huku ukistaajabia utukufu na uumbaji wa MUNGU, hii itakufaa sana.
5. Fanya mazoezi ya kupumzika.
Hapa nazungumzia Yoga, changamsha akili, kutafakari na kupumua kwa kina hii inaweza kusaidia kupunguza viwango vya ujumla vya mafadhaiko.
6. Shiriki burudani na kutafakari vipaumbele vyako.
Sote tunaweza kuwa na kuwa “shughuli nyingi” lakini burudani ni hitaji la afya ya kihisia na kiakili. pata muda wa kupumzika, kutafakari, na kuzingatia mambo mazuri unapoendelea na siku yako, hata mambo madogo usiyaache, ziandike ikiwa unaweza kwa sababu zinaweza kuwa rahisi kusahau. Kisha yatafakari ya baadaye.
7. Kula vyakula vya afya ya ubongo ili kupata afya ya akili yenye nguvu.
Vyakula vinavyoweza kuhimili hisia zako ni pamoja na ulaji wa Samaki wenye mafuta mengi kwa wingi, njugu (walnuts, almonds, korosho na karanga), parachichi, maharagwe, mboga za majani (mchicha, tembele, mnafu), na matunda.
8. Usiupuuze usingizi.
Ni muhimu zaidi kuliko unavyofikiria. Usingizi ndio njia bora ya mwili na akili zetu kuchaji na kuchangamsha mwili na akili. Njia moja ya kupata usingizi bora ni kushiriki kazi na hata mazoezi au kuangalia – TV, kuperuzi simu, kucheza na kompyuta nk, kabla ya kulala. Zingatia kusoma au kusikiliza muziki wa kustarehe pia.
9. Tafuta kusudio la siku yako na maana yake.
Hii huwa ni tofauti kwa kila mtu lakini kutafuta kusudi katika siku yako ni jambo kubwa kwa afya njema ya akili. Unaweza kujaribu mojawapo ya yafuatayo:
Shiriki katika kazi inayokufanya ujisikie kuwa muhimu na wekeza katika mahusiano au tumia muda wako na watu ambao ni muhimu kwako, pia jitolee mambo mbalimbali na hii inaweza kusaidia kuboresha maisha yako na kukufanya uwe na furaha zaidi.
Aidha, kujali wengine inaweza kuthawabisha maisha yako na kuklufanya uwe na maana kama ilivyo katika kukabiliana na changamoto kifikra huku tendo moja zuri au ishara njema zikikupa mustakabali wa afya yako.
10. Pata usaidizi ikiwa una uhitaji.
Ikiwa unahitaji usaidizi, kuna programu nyingi na rasilimali ambazo zinapatikana kwako hivyo usisite kuwaona wataalamu wa masuala ya Afya ili kupata muafaka wa nini unatakiwa ufanye kuepukana na zonge la Afya ya akili.