Pamoja na jitihada zinazoendelea kufanyika juu ya madhara mbalimbali kwa watu wanaotarajia kupata watoto na kupitia ripoti ya utekelezaji wa maazimio ya iliyotolewa jijini Nairobi katika mkutano uliofanyika visiwani Zanzibar, bado afya ya uzazi ni changamoto.
Kauli hiyo, imetolewa na Viongozi mbali mbali wakiongozwa na Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa ripoti hiyo maalumu, juu ya utekelezaji wa maazimio ya Nairobi yaliyowekwa mwaka 2019 ambapo maazimio 12 yalionekana kuwa ni muhimu na yanayohitaji utekelezaji.
Mwenyeji wa Mkutano huo, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi alisema kwa msaada wa washirika wa maendeleo Serikali yake inaendelea kuandaa mfumo wa afya, kujenga miundo mbinu, kuajiri rasilimali watu na kupata vifaa tiba vya afya, ili kutoa huduma bora za mijini na vijijini.
Hata hivyo, Kamisheni ya ufuatiliaji wa maazimio ya Nairobi yenye makamishna 27 na wenyeviti wenza wawili, Jakaya Kikwete na Michaelle Jeans imewachukua miaka mitatu kufuatilia na kufanikisha utekelezaji wa kazi hiyo.