Katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Kerri Kiloh raia wa Scotland aliishi na ujauzito bila kufahamu hadi alipogundua siku nne tu kabla ya kujifungua mtoto wake.

Kwa mujibu wa Daily Record, Kiloh mwenye umri wa miaka 25 alifika katika hospitali ya St. John’s iliyoko Livingstone akiwa na mume wake Kevin ambapo walifika kufahamu kinachomsumbua mwanamke huyo kwa siku kadhaa, ndipo walipopewa habari hiyo nzuri. Lakini alishangaa zaidi baada ya kuambiwa kuwa atajifungua ndani ya siku nne tu  zijazo.

Hata hivyo, habari hiyo iligeuka na kuwapa huzuni kwa wawili hao baada ya madaktari kuwaeleza kuwa mtoto wao atazaliwa kabla ya siku zake kukamilika ikiwa ni wiki 15 kabla (sawa na miezi zaidi ya mitatu kabla).

Baada ya kujifungua, wazazi hao walimpa mtoto wao jina la Karson, lakini madaktari waliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa na asilimia 30 pekee za kuishi. Mtoto huyo aliwekwa kwenye mashine maalum ya kitabibu ya kumsaidia kupumua (ventilator).

mtoto Karson Kiloh akipata matibabu

mtoto Karson Kiloh akipata matibabu

Aprili mwaka jana, wazazi hao walipewa habari njema baada ya kumtembelea mtoto huyo hospitali na kuambiwa kuwa alikuwa anaendelea vizuri na alikuwa na umri wa miezi mitano wakati huo.

Alipofikisha umri wa miezi sita, aliweza kutolewa kwenye mashine hiyo na kuendelea na maisha ya kawaida.

Chanzo: Daily Record

 

TFF Wamlilia Seleman Said ‘Yeltisn’
Mwalimu apigwa risasi kichwani kwa kujisaidia haja ndogo