Baada ya kumaliza michezo ya Kimataifa ya kirafiki katika kipindi cha mapumziko ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ameweka wazi mipango na mikakati ya klabu hiyo kwa mwezi Septemba.
Simba SC ilicheza michezo miwili ya Kimataifa ya Kirafiki nchini Sudan dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na Al Hilal ya Sudan kisha ikamalizia na Arta Soler ya Djibout.
Ahmed Ally ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii (Instagram na Facebook) kuanika mipango ya Simba SC, huku akiitaja michezo ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambapo watacheza dhidi ya Mabingwa wa Malawi Nyasa Big Bullet.
Ahmed Ally ameandika: Ndani ya Mwezi huu wa September tuna mission tatu na zote zinatakiwa kukamilika kwa ukamilifu
Mission ya kwanza ni kumaliza mechi ya tatu nyumbani bila kupoteza ili tuvune alama 9 nyumbani
Jumatano tunacheza dhidi ya KMC kitu tunahitaji ni alama tatu kwenye huu mchezo
Ya pili ni Green City Mission, tuna mechi mbili Mbeya tunahitaji points 6 katika mechi hizi
Msimu uliopita Mbeya tulitoka kapa hatukuvuna hata alama moja lakini safari hii tunataka zote 6
Na ya mwisho ni International Mission, ndani ya mwezi huu tunapaswa kuvuka hatua ya awali na kwenda hatua ya kwanza ya CAF Champions League
Missions zote hizi haziwezi kukamilika bila wana Simba kuunganisha nguvu?
Wa Dar es Salaam tukutane Benjamin Mkapa Jumatano tukamilishe hili la kwanza, then tuianze safari ya Malawi ya kwenda kufanya balaa la kihistoria wakati huo watu wa Nyanda za juu kusini mkijiandaa kuipokea timu yenu??