Kikosi cha polisi usalama barabarani nchini Kenya, kimetangaza kufunga barabara za jijini Nairobi kwa siku ya leo Septemba 5, 2022 ili kupisha usikilizaji wa hukumu ya shauri la kupinga matokeo ya Uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa Kikosi cha usalama barabarani Kaunti ya Nairobi, Vitalis Otieno imesema barabara hizo zitafungwa masaa 2 kabla ya kesi kuanza kusikilizwa.

Wakenya wanasubiri kwa hamu uamuzi wa Mahakama ya Juu wa hii leo kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais, baada ya kupitia siku kadhaa za sintofahamu ya kisiasa nchini humo.

Ahmed Ally aanika mipango ya Simba SC
Wananchi wakataa mapendekezo katiba mpya