Mahakama nchini Pakistan imemhukumu mtu mmoja kwenda jela miezi sita kwa kosa la kuoa mke wa pili bila ya idhini kutoka kwa mke wake, hivyo kuchukua uamuzi huo ambao ni onyo kwa wanaume wenye tabia kama hizo.
Mahakama hiyo ya Lahore pia ilimuamrisha, Shahzad Saqib kulipa faini ya dola 1,900, na kukataa maoni yake kuwa dini ya kiislamu inamruhusu kuoa hadi wake wanne, lakini hoja yake ilikataliwa.
Aidha, Mke wa kwanza wa Sadiq Ayesha, alikuwa amefanikiwa kujitetea kuwa kuoa bila idhini yake ulikuwa ni ukiukaji wa sheria za familia nchini Pakistan, ambapo hata dini hairuhusu kufanya hivyo.
Hata hivyo, nchini Pakistan, wanaume wanaotaka kuoa wanawake kadhaa hufanya hivyo baada ya miaka kadhaa na ni lazima wapate idhini kutoka kwa mke wa kwanza.
Baraza la kiislamu nchini Pakistan ambalo hutoa ushauri wa serikali kuhusu masuala ya kiislamu, mara kwa mara limekosoa sheria za familia nchini humo.