Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika, Obadele Kambon amesema kuwa hajawahi kujutia hatua yake ya kuhamia nchini Ghana tangu mwaka 2008.
Amesema kuwa tayari alishaapa kutorejea tena nchini humo baada ya tukio la kukamatwa kwake analoamini kwamba lilichochewa na ubaguzi wa rangi.
Kambon ambaye kwasasa ameanza upya maisha katika taifa ambalo lilikuwa kitovu cha biashara ya utumwa amesema kuwa anafurahia uhuru alioukosa nchini Marekani alikozaliwa.
Aidha, amesema kuwa hana hofu ya kukamatwa na polisi tena au cha kuogofya nchini Ghana, lakini anamkumbuka sana mwanaye wa kiume, Tamara Rice aliyekuwa na umri wa miaka 12, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi katika bustani ya Cleveland, Ohio nchini Marekani, mwaka 2014 akiwa anacheza na bunduki bandia ambayo polisi walidhani ya kweli.
Kifo cha Rice kilisababisha maandamano makubwa mjini Cleveland, na kuwa mwanzo wa vuguvugu la kupigania uhuru wa watu weusi maarufu kama ‘Black Lives Matter.’
Hata hivyo, ameongeza kuwa tangu alipohamia Ghana, amegundua kuwa hajawahi kuhisi kuwa ni mhanga wa ubaguzi wa rangi wala kutukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake.
-
Rais Museveni adai hana mpango wa kustaafu mapema
-
Kenya kuiwakilisha Afrika ‘UN’
-
Rais Museveni, Kagame wamaliza tofauti zao