Kuoa au kuolewa ni jambo la kheri mbele ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa watu wengi huchukulia jambo hilo kimzaa mzaa, wanawake wengi wakifikia umri fulani bila ndoa hupata msongo wa mawazo na hilo humfanya kutaka sana kuolewa hali inayopelekea yeyote atayekuja machoni mwake kumtakia kumuoa kukubaliana nae.
Kuna mambo mengi kwenye ndoa yakiwemo furaha, uchungu, uvumilivu, mateso, chuki, dhiki, utajiri, umaskini na mengine mengi, wengi wetu huwaza kuolewa kwa kuichekelea sherehe kubwa inayofanywa na ndugu jamaa na marafiki pindi wanapokabidhisha mke kwa mume.
Hivyo hebu tuangalia aina tata tano za ndoa kisha fanya tathmini ni ndoa ipi utaangukia.
- Ndoa ya mimba, hii ni ndoa ambayo hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje, au muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa dhati, muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani, hii huvunjika mtoto akizaliwa au akifikisha mwaka.
- Ndoa ya mali, mara nyingi ndoa ya namna hii ni ndoa ambayo muoaji na muolewaji hupishana kwa miaka mingi sana miaka 18 au 28, au 65 na 70, mara nyingi mabinti wadogo hupendelea kuolewa na wazee wanaojiweza kifedha yaani wazee wenye mali za kutosha, aina hii ya ndoa mara nyingi wanaume hujikuta wakilea watoto ambao sio wa kwao.
- Ndoa ya kwa sababu, aina hii ya ndoa muoaji au muolewaji anaingia kwenye ndoa ilimradi aonekane katika jamii kuwa nayeye kaoa au kuolewa, huwa hazina utii wala upendo wa dhati. Ndoa ya aina hii ikifika miaka 4 huvunjika kwasababu mke au mume huishi kwa mazoea.
- Ndoa ya upendo, aina hii ya ndoa huitwa ndoa zilipendwa kwani ziliisha tangu mwaka 1978 kabla ya vita ya kagera ambapo muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu , ndoa ya namna hii hudumu siku zote.
- Ndoa kutuma, aina hii ya ndoa hufungwa ilimradi muolewaji au muoaji apate kitu au vitu fulani, ndoa ya namna hii hudumu kwa muda fulani mpaka malengo ya mmoja wapo yatimie.