Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amethibitisha tukio la vifo vya watu watatu waliofariki kufuatia ajali ya lori lililokuwa limebeba gesi, kugongana uso kwa uso na lori katika Kijiji cha Maili Kumi Wilaya ya Handeni barabara ya Segera Mkoani Tanga.

Ajali hiyo inayodaiwa kutokea majira ya usiku wa kuamkia Januari 6, 2023 ilisababisha mlipuko wa moto ulitokana na gesi ambapo waliofariki waliteketezwa na moto akiwemo Dereva wa lori la gesi na watu wawili ambao bado hajatambulika walikuwa ndani ya Lori aina ya Fuso.

Moja kati ya matukio ya ajali za Barabarani ambayo yalisababisha moto kuwaka. Picha ya New Straight Times.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema, kutokana na moto huo barabara hiyo ikawa haipitiki na kusababisha foleni ya magari yaliyokuwa yakipita barabarani na walishindwa kuwaokoa watu waliokuwamo ndani ya magari kutokana na moto kuwa mkubwa.

Hata hivyo, Kamanda Mwaibambe amesema baada ya tukio hilo moto ulizimwa na barabara ikaanza kutumika kama kawaida na kubainisha kuwa bado wanafuatilia majina ya marehemu na watayatoa mara baada ya taratibu kukamilika huku uchunguzi juu ya ajali hiyo ukiendelea.

Kahawa yawatokea puani Viongozi wa ushirika
BoT yatahadharisha umma pesa za mtandao