Zaidi ya abiria 233 wamefariki Dunia, na wengine 900 kujeruhiwa baada ya treni mbili za abiria kugongana katika Jimbo la Odisha nchini India .
Akizungumza na vyombo vya Habari kuhusu ajali hiyo, Mtendaji Mkuu wa Jimbo la Odisha, Pradeep Jena amesema idadi ya waliokufa inatarajiwa kuongozeka.

Amesema, zaidi ya magari 200 ya kubebea wagonjwa yalitumika katila uokozi na utoaji wa huduma chini ya madaktari wa ziada 100 waliofika kuwaongezea nguvu wengine 80 waliokuwepo.