Dereva wa Bodaboda, Cosmas Samweli (36), mkazi wa Mtaa wa Kilongo B kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro, ameuwawa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kutobolewa macho na watu wasiojulikana .

Akizungumzia tukio hilo, mdogo wa marehemu Huruma Samweli amesema Mei 31, 2023 Cosmas alimuaga mkewe kuwa anaelekea shambani eneo la CCT Forest Manispaa ya Morogoro.

Amesema, mara baada ya kuondoka mumewe hakurejea tena hadi Juni mosi, 2023 walipoukuta mwili wake umetekelezwa eneo la msitu huo ukiwa na majereha huku macho yake kutobolewa na pikipiki haikuwepo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kilongo B, Paul Laurence amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kwa sasa wanaanza msako kuwatafuta vijana wote ambao wanakaa vijiweni na kuvuta bangi ili waweze kuchukuliwa hatua kwani huenda ikawa sababu ya matukio kama hayo kutokea katika mtaa wake.

Ugonjwa wa Marburg wamalizika Kagera - Serikali
Ajali: Treni zagongana zaidi ya 233 wafariki