Watu wasiopungua 45, wamenusurika kifo huku wengine 13 wakipata majeraha wakati basi la kifahari lilipotumbukia kwenye mtaro wa maji katika barabara ya Ejule-Ochadamu iliyopo Halmashauri ya Ofu, Jimbo la Kogi nchini Nigeria.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha Shirikisho la Sekta ya Jimbo la Kogi (FRSC), Stephen Dawulung amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema tukio hilo lilitokea majira ya saa nane mchana Septemba 6, 2022.

Ajali ya basi la Guo iliyotokea hii leo Septemba 6, 2022.

Amesema, majeruhi hao 15 walipelekwa katika Hospitali ya Grimard, Anyigba na Hospitali ya Holy Memorial kwa matibabu huku walionusurika wakiruhusiwa kuendelea na safari.

Kufuatia ajali hiyo, Dawulung amewaonya madereva kuacha tabia ya kuendesha magari kwa mwendo kasi, kwani mara zote huwa ni chanzo cha ajali na vifo kwenye barabara kuu.

Inadaiwa kuwa Dereva wa basi hilo alipoteza mwelekeo kutokana na hitilafu ya breki na chanzo cha kutumbikiza basi mtaroni kilitokana na mwendokasi.

Makamishna wa Ardhi wakalia kuti kavu
Kenya: Zuio jipya la uapisho wa Ruto latupiliwa mbali na Mahakama