Chama tawala nchini Uingereza, Conservative kimemtangaza Liz Truss kuwa Kiongozi mpya wa chama hicho ambaye pia atachukua wadhifa wa Waziri Mkuu kurithi Boris Johnson aliyejiuzulu miezi miwili iliyopita.

Liz Truss, ambaye ni Waziri wa Mambo ya kigeni ametangazwa hii leo Septemba 5, 2022 akimshinda mpinzani wake kwa kupata idadi kubwa ya kura za wananchama wa Conservative.

Katika kipindi cha wiki nane zilizopit, wanasiasa hao walizunguka nchi nzima kuomba kura za wanachama wakiahidi kushughulikia matatizo makubwa ya kiuchumi yanayoikabili Uingereza, ikiwemo kupanda kwa bei za nishati.

Truss, sasa anarithi Taifa lenye uchumi unaoelekea kudorora na atakuwa na kibarua kigumu cha kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha, zilizochochea mamia kwa maelfu ya wafanyakazi kugoma wakidai nyongeza ya mshahara.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 06, 2022
Rais Samia awa 'Suprise' wasafiri ndani ya Boti