Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hii leo Agosti 5, 2022 ametumia usafiri wa boti ya M.V Kilimanjaro 4 kutoka Zanzibar kwenda jijini Dar es Salaam akitokea Visiwani humo katika ziara yake ya kikazi.

Ametumia boti ya katika bandari ya Malindi kwenda jijini Dar es Salaam akiambatana na viongozi wengine pamoja na abiria.
Rais Samia, akiwa ndani ya usafiri huo aliwasalimia na abiria wenzake (Wananchi), waliokuwa wakisafari pamoja.

Akiwasalimia Wananchi, Rais Samia aliwatakia safari njema na kusema, “Jamani hamjambo, kwema, hali zenu, Mungu atusafirishe salama,” aliongea huku akiwa na nyuso ya furaha kama ilivyokuwa kwa wananchi ndani ya Boti hiyo.

Rais Samia alihudhuria matukio tofauti ikiwemo kufunga tamasha la Kizimkazi lililokuwa likifanyika katika viwanja vya Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Rais Samia akisaini kitabu cha kumbukumbu ndani ya Boti ya M.V Kilimanjaro 4, aliyosafiri nayo kutoka Zanzibar hadi jijini Dar es Salaam.

Rais Samia alikuwepo Zanziba kwa ziara ya kikazi, ambapo alizinduamiradi mbalimbali na litoa pole kwa familia ya Rais mstaafu wa awamu ya Pili ya Zanzibar, Ali Hassan Mwinyi kufuati kifo cha mtoto wake, Dkt. Hassan Ali Mwinyi.

Mrithi wa Boris Johnson na 'Conservative' apatikana
Kamati ya Bunge yaridhishwa utekelezaji 'Timiza Malengo'