Hospitali Teule ya Mugana iliyoko Wilayani Misenyi Mkoani Kagera, imefanikiwa kumfanyia upasuaji kijana mmoja mgonjwa akili mkazi wa Kyerwa mkoani humo nakumkuta na vifaa mbalimbali tumboni ikiwemo mswaki, kijiko, betri ndogo, kalamu, viberiti vya gesi, mfuko, vitambaa pamoja na mkonga wa mashine ya kunyolea ndevu.
Aidha, Mganga Mkuu Wa Wilaya Missenyi Dkt. Khamis Abdallah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakumtaja mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji nakukutwa vitu hivyo tumboni kwake kuwa ni Robert Novato mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Kyerwa Mkoani Kagera nakwamba ni mgonjwa wa akili kwasasa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Mugana
Hata hivyo, baadhi ya wananchi Wilayani Misenyi wanajiuluza ni kwa jinsi gani vitu hivyo viliingia tumboni, licha ya historia ya kijana huyo kujulikana kwamba ni mgonjwa wa akili Wengine wakiamini kuwa alimeza vitu hivyo mwenyewe Wengine wakiamini katika ushirikina.
-
Uwekezaji kutoka China kuifikisha Tanzania uchumi wa kati
-
BREAKING: Rais Magufuli akizungumza na wananchi Ukerewe
-
Jafo awasilisha muswada wa kulitangaza Jiji la Dodoma