Mshambuliaji wa Newcastle Utd Aleksandar Mitrovic amefungiwa kucheza michezo mitatu, baada ya kamati ya nidhamu ya chama cha soka nchini England FA, kumkuta na hatia ya kupiga kiwiko akiwa mchezoni.
Mshambuliaji huyo kutoka nchini Serbia, alifanya tukio hilo katika mchezo wa ligi ya nchini England mwishoni mwa juma lililopita, kwa kumpiga kiungo wa West Ham Utd Manuel Lanzini. Katika mchezo huo West Ham Utd walikubali kunyukwa mabao matatu kwa sifuri.
-
Haji Manara afichua siri ya muonekano wa kikosi cha Simba SC
-
Diego Costa kusajiliwa kwa mkopo Hispania
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hakuadhibiwa na mwamuzi wa mchezo huo, kutokana na kutoona kitendo cha kumpiga mchezaji wenzake, jambo ambalo liliiamsha kamati ya nidhamu ya FA na kufuatilia kwa kina tukio hilo kwa picha za televisheni.
Mitrovic atakosa michezo ya ligi ya England dhidi ya Swansea City, Stoke City na Brighton.