FC Barcelona wamepanga kuitega Arsenal, kufuatia ofa iliyotumwa Camp Nou kutoka kaslkazini mwa jijini London kwa lengo la usajili wa kiungo wa kituruki Arda Turan.

Arsenal wametuma ofa ya Pauni milioni 25, ambayo wanaamini itatosha kumng’oa Turan Camp Nou, kufuatia kutokuwepo kwenye mipango ya meneja wa sasa wa The Catalan, Ernesto Valverde Tejedor.

Barca amepanga kufanya biashara ya kutaka kumtumia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye amekua akiwindwa na Arsenal kwa muda mrefu, kama sababu ya kubadilishana na Mesut Ozil.

Barca wamejipanga kutumia mbinu hiyo, kufuatia mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Liverpool Philippe Coutinho, kushindwa kuzaa matunda, licha ya mazungumzo kati yao na majogoo wa jiji kufanyika kila kukicha.

Gazeti la El Mundo Deportivo limetoka na taarifa zinazodai kuwa, meneja wa Barca Ernesto Valverde anaamini endapo atafanikiwa kumpata Ozil, atakua ametimiza lengo la kukiweka vyema kikosi chake hususan katika kipindi hiki ambacho ameanza vizuri ligi ya nchini Hispania.

Ozil amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Arsenal, na bado hajasaini mkataba mpya, jambo ambalo linachukuliwa FC Barcelona kama njia sahihi ya kumpata kwa urahisi.

Aleksandar Mitrovic atupwa jela kwa wiki tatu
Liverpool yakamilisha usajili wa Chamberlain