Mkali wa ‘Seduce Me’, Ali Kiba ameweka wazi kuwa ameguswa na uwezo wa kuimba wa Lavalava ambaye ni msanii wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na Diamond Platinumz.

Ali Kiba alifunguka wiki hii kupitia The Playlist ya 100.5 Times FM kuwa Lava Lava ni msanii ambaye ni mkali na anamkumbusha wakali waliowahi kuwa na mtindo kama wake akimtaja Alicom.

“Ngoma nyingine… nilikuwa naisikia, napenda sana kuisikiliza vilevile ni ya Lavalava (anacheka). Inaitwa Bora tuachane, naipenda sana ile,” alisema Ali Kiba alipotakiwa na Lil Ommy kuchagua ngoma ya pili kati ya tano anazozikubali zaidi.

“Amenikumbusha kuna ile Bongo Fleva ya zamani tulikuwa tunaimba. Kulikuwa na akina Alicom. Wasanii wa zamani wote unaowajua, kulikuwa kuna styles (mitindo) walikuwa wakifanya wanatwist sauti. Napenda sana jinsi anavyotwist sauti. Ameimba vizuri, amenifurahisha sana kwenye ile ngoma,” alifunguka

‘Bora Tuachane’ ni wimbo wa kwanza wa Lavalava uliomtambulisha vyema kama msanii mpya wa lebo ya WCB. Hivi karibuni ameachia wimbo mwingine unaoitwa ‘Dede’.

Mbali na Lavalava, Ali Kiba amewahi kuonesha kumkubali Ray Vany wa WCB na hata kuimba vipande vya nyimbo zake na kupost kwenye Instagram.

Kiba ameendeleza ubabe kwenye mtandao wa YouTube kupitia wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ ambao umeangaliwa zaidi ya mara milioni tatu ndani ya muda mfupi. Hadi sasa umeshikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa gumzo (trending) Tanzania na Kenya.

Sheria kuchukua mkondo wake wapiga picha utupu
Aleksandar Mitrovic atupwa jela kwa wiki tatu