Kupitia kesi inayomkabili msanii Amber Lulu baada ya picha zake za nusu utupu kuvuja, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa watanzania wengine wenye tabia kama hiyo kuchukuliwa hatua kali kwa kuvunja sheria za mtandaoni.

Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi SACP, Lazaro Mambosasa.

”Hilo ni kosa kama kosa lingine, ni uvunjaji wa sheria za makosa ya kimtandao, mtu yeyeote akija kulalamika Jeshi la Polisi halitamfumbia macho, kwa sababu vitendo hivyo ni udhalilishaji wa utu wa mtu wa hali ya juu na haviwezi kuvumilika, ukidhibitika unafanya kitendo hicho jeshi la polisi litakuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria,” amsema Mambosasa.

Vitendo vya upigwaji wa picha za utupu na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii vimekuwa vikishamiri nchini Tanzania, ambapo hivi karibuni msanii Amber Lulu alifikishwa katika kituo cha polisi cha Ubungo kwa kosa hilo.

Wasanii wengine wenye tabia kama hizo za kutuma picha za uchi ni kama Gigy Money, Sanchoka, na watanzania wengine wenye tabia kama hiyo na bado hawajapata umaarufu kwani sheria lazima ichukue mkondo wake endapo tabia kama hizo zikijitokeza.

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 1, 2017
Ali Kiba amvulia kofia Lavalava wa WCB