Kiungo wa Liverpool, Alexis Mac Allister anaweza kukumbana na adhabu ya Chama cha Soka England (FA) baada ya kudai kuwa mwamuzi Simon Hooper alichangia wapoteza mechi dhidi ya Tottenham mwishoni mwa juma lililopita.

Liverpool ilipata bao halali kipindi cha kwanza lililowekwa kiamiani na Luis Diaz kabla ya kufungwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu England huku wakiwa wachezaji tisa.

Hata hivyo, Mac Allister raia wa Argentina alitoa hasira zake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuona posti ya Instagram ya beki wa Spurs, Cristian Romero akisifu ushindi huo.

Mabosi wa FA huenda wakampiga faini Mac Allister kutokana na kauli aliyotoa mtandaoni akimkosoa mwamuzi kufuatia uamuzi wa ajabu wa VAR.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alifungiwa mechi mbili msimu uliopita baada ya kumkosoa mwamuzi Paul Tierney katika ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Spurs, hivyo kiungo huyo huenda akakumbana na adhabu.

Mwishoni mwa juma lililopita Liverpool ililalamika baada ya bao halali kukataliwa na mwamuzi Darren England anayesimamia VAR.

Chama cha Waamuzi (PGMOL) kilikiri dosari katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England na kuomba radhi.

Klopp alicharuka baada ya mechi kumalizika akisema: “Sijawahi Kuona mechi kama hii yenye mazingira yasiyo na haki. Uamuzi wa ajabu kabisa.

“Kadi nyekundu ya kwanza, hata kadi ya njano ya Diogo Jota, bao la alilofunga Diaz ni halali.”

Mfumo ikolojia kutumika Vijijini kuyakabili mabadiliko Tabianchi
Kamchape waivuruga jamii, Chongolo aingilia kati