Algeria imefungia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter nchi nzima kwa lengo la kulinda mitihani ya kitaifa isivurugwe.

Nchi hiyo imechukua uamuzi huo baada ya kushuhudiwa maswali na karatasi za mitihani zikiwa zimevuja na kusambaa kwa kasi kupitia mitandao hiyo.

Serikali ya nchi hiyo imesema kuwa mitihani ya awali ilivuja na kubatilishwa hivyo wameamua kufunga mitandao hiyo ili wanafunzi wasiendelee kulishwa mawazo ya mitihani hiyo iliyovuja wakati wanajiandaa kufanya mitihani mingine siku za hivi karibuni.

Mtandao wa Independent wa Uingereza umeripoti kuwa mwezi uliopita, Polisi nchini humo walikamata watu kadhaa katika harakati za kutaka kubaini jinsi ambavyo mitihani ya masomo ya juu ya sekondari ilivyoweza kuingia mitandaoni.

Jana, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia wan chi hiyo alithibitisha kuwa kufungwa kwa mitandao hiyo ya kijamii kuna uhusiano wa moja kwa moja na kuvuja kwa mitihani hiyo.

 

Nape ataka CCM ifumuliwe, asema imejaa urasimu
Video: Jeshi la Wananchi Tanzania limekanusha taarifa za kuibwa kwa kifaru