Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja aliyekamatwa baada ya kuiba mafaili katika ofisi ya Afisa Mtafiti wa Mazingira wa Kata ya Bomambuzi, Abdalah Hussein.

Kwa mujibu wa Hussein, mtuhumiwa huyo alipokamatwa akiwa na mafailihayo akijaribu kutoka nje ya ofisi hiyo, alidanganya kuwa alitumwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Mtu huyo alibainika kuwa alidanganya na kusingizia kutumwa na Mkuu huyo wa Mkoa.

Afisa huyo alieleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa na msamalia mwema aliyemshtukia wakati anatoka ofisini.

“Niliporudi ofisini, nilimkuta mtuhumiwa na baada ya kumuuliza kwa nini alibeba mafaili, akadai kuwa katumwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,” alisema Hussein.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro alieleza kuwa bado mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi.

Chanzo: Mwananchi

Jamal Malinzi Ampongeza Jakaya Mrisho Kikwete
Tai wapewa mafunzo kuteka ndege zisizo na rubani