Diane Rwigara, aliyekuwa mpinzani wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwenye mchakato wa uchaguzi uliopita amepotea. Ndugu zake wamelitupia lawama jeshi la polisi wakilihusisha na tukio hilo.
Mjomba wa mwanasiasa huyo ameiambia BBC kuwa watu waliokuwepo wakati anachukuliwa wanadai alifungwa pingu na kuondoka na wanafamilia watano ambao wote walifikishwa kwenye kituo cha polisi.
Hata hivyo, msemaji wa jeshi la polisi la nchi hiyo, Theos Badege amekanusha taarifa hizo akieleza kuwa jeshi hilo halikumkamata bali linachokifanya hivi sasa ni kumtafuta.
Mwili wa Manji wapumulia vyuma
Ne-Yo kuzunguka na Diamond kwenye ziara yake UK
“Hao wanasema wanapotaka wao wawepo, na kwasababu kazi yetu ilikuwa kuwatafuta ambayo ni sehemu ya uchunguzi kama nilivyosema awali, hatufahamu walipo,” alisema Badege.
Msemaji huyo wa jeshi hilo ameongeza kuwa walichokifanya ni kushikilia kompyuta na baadhi ya vifaa vya kielektroniki vya Rwigara kwa lengo la kuvitumia kusaidia uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.