Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amemchagua Jenerali wa zamani wa Jeshi la nchi hiyo, Constantino Chiwenga kuwa Makamu wa Rais.
Jenerali Chiwenga ambaye aling’atuka uongozi wa Jeshi wiki iliyopita ndiye aliyeongoza harakati za jeshi la nchi hiyo zilizopelekea Robert Mugabe kujiuzulu.
Alikula kiapo cha kuwa makamu wa Rais jana katika Ofisi ya Rais wa nchi hiyo ambaye amesisitiza kuwa ataendelea kuwasaka watu wabaya walio ndani ya mfumo wa chama na Serikali.
Ripoti zinaeleza kuwa Rais Mnangagwa amepanga kuwahusisha Polisi wa Kimataifa (Interpol) kwenye msako wa watu hao ‘wabaya’ wanaotajwa kuwa walikuwa wamemzunguka Mugabe.