Mchezaji Hiannick Kamba, aliyetangazwa amekufa katika ajali ya gari mwaka 2016 amekutwa yupo hai.
Kwa mujibu wa gazeti la Bild la nchini Ujerumani, Kamba kwa sasa anafanya kazi katika kampuni ya Nishati mjini Ruhr nchini Ujerumani.
Kamba mwenye umri wa miaka 33, aliwahi kuchezea FC Schalke 04 ambapo Januari 09 mwaka 2016,taarifa zilitolewa kuwa amekufa katika ajali ya gari nchini DRC.
Klabu yake aliyokuwa anaichezea wakati huo VfB Hüls ya Ujerumani ilithibitisha kifo chake.
Kamba ametoa maelezo ya kilichotokea na kusema kwamba marafiki zake walimtelekeza usiku na kuchukua simu yake, Hati ya Usafiri na fedha na baadae akatoa taarifa katika Ubalozi wa Ujerumani nchini DRC lakini hakufanikiwa kutokana na kukosa vielelezo.
Inaelezwa kuwa mke wake alitoa taarifa kuwa mume wake amekufa lakini mwaka 2018 akiwa nchini Ujerumani, Kamba alijitokeza mbele ya vyombo vya Usalama na kusema kuwa yupo hai ila amezushiwa kifo.
Mwendesha mashtaka wa serikali Anette Milk amesema wawili hao wameshitakiwa kwa tuhuma ya udanganyifu.