Bodi ya ligi nchini Ujerumani (DFL) imethibitisha kuwa ligi kuu ya soka nchini humo (Bundesliga), inatarajiwa kuendelea Mei 15, baada ya kusimama kupisha vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Bodi hiyo imethibitisha taarifa za kurejea kwa ligi, kufutia kauli iliyotolewa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, alipokua akizungumzia maendeleo ya hali ya maambukizi nchini humo jana Jumatano.

Hata hivyo bado haijaelezwa kama ligi ya Ujerumani na ligi nyingine za madaraja ya chini zitarejea kwa kufuata ratiba ilivyokua inaonekana kabla ya kusimamishwa mwezi Machi mwaka huu.

Ligi ya Ujerumani ilisimama ikiwa kwenye mzunguuko wa 26.

Wakati ligi ya Ujerumani inasimamishwa kupisha janga la Corona, mabingwa watetezi FC Bayern Munich walikua kileleni mwa msimamo kwa kufikisha alama 55, wakifuatiwa na Borussia Dortmund wenye alama 51 na RB Leipzig wanashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 50.

Uhamisho wa Fernandes waanza kuchunguzwa FIFA
Aliyetangazwa kufa 2016 bado yuhai