Rais wa Chama cha Soka nchini Uturuki, Nihat Ozdemir amesema taifa hilo liko tayari kwa mchezo wa fainali Ligi ya Mabingwa barani Ulaya  katika tarehe itakayopangwa ndani ya mwezi Agosti mwaka huu.

Uwanja wa Atatürk Olympic uliopo katika jiji la Istanbul ndiyo uliopangwa kuamua fainali hiyo kabla ya michezo yote kusitishwa mwezi Machi kutokana na janga la virusi vya Corona.

Nihat amesema ligi kuu ya nchi hiyo itaendelea kuanzia Juni 12 mwaka huu, lengo likiwa ni kumaliza michezo yote ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

Tayari klabu za Paris Saint-Germain (Ufaransa), RB Leipzig (Ujerumani), Atalanta (Italia) na Atlético Madrid (Hispania) zimeshatinga hatua ya robo fainali, baada ya kushinda michezo ya hatua ya 16, kabla ya kusimamishwa kwa michiano hiyo mwezi Machi.

Klabu ambazo zilitarajiwa kukamilisha safari ya kutinga robo fainali kwa kukamilisha michezo ya mkondo wa pili hatua ya 16 bora ni Barcelona (Hispani) dhidi ya SSC Napoli (Italia), ambapo katika mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizo zilimaliza kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Olympic Lyon (Ufaransa) dhidi ya Juventus (Italia), katika mchezo wa mkondo wa kwanza Lyon walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Chelsea (England) dhidi ya Bayern Munich (Ujerumani), mchezo wa mkondo wa kwanza The Bavarians walipata ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Real Madrid (Hispania) dhidi ya Manchester City (England), mchezo wa kwanza City walipata ushindi wa mabao mawili kwa moja.

UEFA wametoa tarehe za makadirio endapo hali itarejea kuwa shwari, ili  michezo ya hatua ya 16 bora ikamilishwe, na kuendelea kwa hatua nyingine hadi fainali.

UEFA wamekadiria michezo iliyosalia kuchezwa kati ya Juni 25 hadi  Agosti 28/2019

Mwanri: "Tunakuja na kitu kinaitwa kubamiza corona"
Walevi wageukia 'Soseji moja na bia mbili' kukabili zuio la kufungwa bar